27 Ibrahimu akatwaa kondoo na ng’ombe akampa Abimeleki, na hao wawili wakafanya mapatano.
28 Ibrahimu akaweka wana kondoo wa kike saba peke yao.
29 Abimeleki akamwambia Ibrahimu, Hawa wana kondoo wa kike saba, uliowaweka peke yao, maana yake nini?
30 Akasema, Hawa wana kondoo wa kike saba utawapokea mkononi mwangu, wawe ushuhuda ya kuwa ni mimi niliyekichimba kisima hiki.
31 Kwa hiyo akapaita mahali pale Beer-sheba, kwa sababu waliapa huko wote wawili.
32 Basi wakafanya mapatano huko Beer-sheba. Abimeleki, na Fikoli mkuu wa jeshi lake, wakaondoka wakarudi hata nchi ya Wafilisti.
33 Ibrahimu akapanda mkwaju huko Beer-sheba, akaliitia huko jina la BWANA Mungu wa milele.