5 Naye Bilha akapata mimba, akamzalia Yakobo mwana.
6 Raheli akasema, Mungu amenipa haki yangu, naye amesikia sauti yangu, akanipa mwana. Kwa hiyo akamwita jina lake Dani.
7 Bilha, mjakazi wa Raheli, akapata mimba tena, akamzalia Yakobo mwana wa pili.
8 Raheli akasema, Kwa mashindano makuu nimeshindana na ndugu yangu, nikashinda. Akamwita jina lake Naftali.
9 Lea alipoona ya kuwa ameacha kuzaa, alimtwaa Zilpa, mjakazi wake, akampa Yakobo kuwa mkewe.
10 Zilpa, mjakazi wa Lea, akamzalia Yakobo mwana.
11 Lea akasema, Bahati njema! Akamwita jina lake Gadi.