20 Yakobo akasimamisha nguzo juu ya kaburi lake, ndiyo nguzo ya kaburi la Raheli hata leo.
21 Kisha akasafiri Israeli akapiga hema yake upande wa pili wa mnara wa Ederi.
22 Ikawa Israeli alipokuwa akikaa katika nchi ile, Reubeni akaenda akalala na Bilha, suria wa babaye; Israeli akasikia habari.Basi hao wana wa Yakobo walikuwa kumi na wawili.
23 Wana wa Lea ni Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Yakobo, na Simeoni, na Lawi, na Yuda, na Isakari, na Zabuloni.
24 Wana wa Raheli, ni Yusufu na Benyamini.
25 Wana wa Bilha, kijakazi wa Raheli, ni Dani na Naftali.
26 Wana wa Zilpa, kijakazi wa Lea, ni Gadi na Asheri. Hawa ndio wana wa Yakobo aliozaliwa katika Padan-aramu.