20 Hawa ni wana wa Seiri, Mhori, wenyeji wa nchi ile; Lotani, na Shobali, na Sibeoni, na Ana,
21 na Dishoni, na Eseri, na Dishani. Hao ndio majumbe waliotoka katika Wahori, wana wa Seiri, katika nchi ya Edomu.
22 Na wana wa Lotani, ni Hori, na Hemamu; na umbu lake Lotani ni Timna.
23 Na hawa ni wana wa Shobali, Alvani, na Manahathi, na Ebali, na Shefo, na Onamu.
24 Na hawa ni wana wa Sibeoni, Aya, na Ana; ni yule Ana aliyeona chemchemi za maji ya moto katika jangwa, alipokuwa akichunga punda za Sibeoni babaye.
25 Na hawa ni wana wa Ana, Dishoni, na Oholibama, binti Ana.
26 Na hawa ni wana wa Dishoni, Hemdani, na Eshbani, na Ithrani, na Kerani.