22 Na wana wa Lotani, ni Hori, na Hemamu; na umbu lake Lotani ni Timna.
23 Na hawa ni wana wa Shobali, Alvani, na Manahathi, na Ebali, na Shefo, na Onamu.
24 Na hawa ni wana wa Sibeoni, Aya, na Ana; ni yule Ana aliyeona chemchemi za maji ya moto katika jangwa, alipokuwa akichunga punda za Sibeoni babaye.
25 Na hawa ni wana wa Ana, Dishoni, na Oholibama, binti Ana.
26 Na hawa ni wana wa Dishoni, Hemdani, na Eshbani, na Ithrani, na Kerani.
27 Na hawa ni wana wa Eseri, Bilhani, na Zaawani, na Akani.
28 Na hawa ni wana wa Dishani, Usi, na Arani.