24 Na hawa ni wana wa Sibeoni, Aya, na Ana; ni yule Ana aliyeona chemchemi za maji ya moto katika jangwa, alipokuwa akichunga punda za Sibeoni babaye.
25 Na hawa ni wana wa Ana, Dishoni, na Oholibama, binti Ana.
26 Na hawa ni wana wa Dishoni, Hemdani, na Eshbani, na Ithrani, na Kerani.
27 Na hawa ni wana wa Eseri, Bilhani, na Zaawani, na Akani.
28 Na hawa ni wana wa Dishani, Usi, na Arani.
29 Hawa ndio majumbe waliotoka katika Wahori; jumbe Lotani, jumbe Shobali, jumbe Sibeoni, jumbe Ana,
30 jumbe Dishoni, jumbe Eseri jumbe Dishani. Hao ndio majumbe waliotoka katika Wahori, kwa habari za majumbe yao, katika nchi ya Seiri.