31 Na hawa ndio wafalme waliomiliki katika nchi ya Edomu, kabla ya kumiliki mfalme ye yote juu ya wana wa Israeli.
32 Bela wa Beori alimiliki katika Edomu, na jina la mji wake ni Dinhaba.
33 Akafa Bela, akamiliki Yobabu mwana wa Zera, wa Bosra, badala yake.
34 Akafa Yobabu, akamiliki Hushamu, wa nchi ya Watemani, badala yake.
35 Akafa Hushamu, akamiliki Hadadi wa Bedadi badala yake, naye ndiye aliyepiga Midiani katika nyika ya Moabu, na jina la mji wake ni Avithi.
36 Akafa Hadadi, akamiliki Samla wa Masreka badala yake.
37 Akafa Samla, na Shauli wa Rehobothi, ulio karibu na mto, akamiliki badala yake.