33 Akafa Bela, akamiliki Yobabu mwana wa Zera, wa Bosra, badala yake.
34 Akafa Yobabu, akamiliki Hushamu, wa nchi ya Watemani, badala yake.
35 Akafa Hushamu, akamiliki Hadadi wa Bedadi badala yake, naye ndiye aliyepiga Midiani katika nyika ya Moabu, na jina la mji wake ni Avithi.
36 Akafa Hadadi, akamiliki Samla wa Masreka badala yake.
37 Akafa Samla, na Shauli wa Rehobothi, ulio karibu na mto, akamiliki badala yake.
38 Akafa Shauli, akamiliki Baal-hanani, mwana wa Akbori, badala yake.
39 Akafa Baal-hanani, mwana wa Akbori, akamiliki Hadadi badala yake; na jina la mji wake ni Pau; na jina la mkewe ni Mehetabeli, binti Matredi, binti Mezahabu.