1 Yakobo akawaita wanawe, akasema, Kusanyikeni, ili niwaambie yatakayowapata siku za mwisho.
2 Kusanyikeni, msikie, enyi wana wa Yakobo,Msikilizeni Israeli, baba yenu.
3 Reubeni, u mzaliwa wangu wa kwanza,Nguvu zangu, na malimbuko ya uwezo wangu.Umewapita wengine kwa ukuu na kwa nguvu.
4 Umeruka mpaka kama maji, basi usiwe na ukuu,Kwa sababu ulikipanda kitanda cha baba yako,Ukakitia unajisi; alikipandia kitanda changu.