13 Zabuloni atakaa pwani ya bahari,Naye atakuwa kama pwani za kuegesha merikebu,Na mpaka wake utakuwa kando ya Sidoni.
14 Isakari ni punda hodari,Ajilazaye kati ya mazizi ya kondoo;
15 Akaona mahali pa raha, kuwa pema,Na nchi, ya kuwa ni nzuri,Akainama bega lake lichukue mizigo,Akawa mtumishi kwa kazi ngumu.
16 Dani atahukumu watu wake,Kama moja ya makabila ya Israeli;
17 Dani atakuwa nyoka barabarani,Bafe katika njia,Aumaye visigino vya farasi,Hata apandaye ataanguka chali.
18 Wokovu wako nimeungoja, Ee BWANA.
19 Gadi, jeshi litamsonga,Lakini atawasonga wao mpaka visigino.