14 Isakari ni punda hodari,Ajilazaye kati ya mazizi ya kondoo;
15 Akaona mahali pa raha, kuwa pema,Na nchi, ya kuwa ni nzuri,Akainama bega lake lichukue mizigo,Akawa mtumishi kwa kazi ngumu.
16 Dani atahukumu watu wake,Kama moja ya makabila ya Israeli;
17 Dani atakuwa nyoka barabarani,Bafe katika njia,Aumaye visigino vya farasi,Hata apandaye ataanguka chali.
18 Wokovu wako nimeungoja, Ee BWANA.
19 Gadi, jeshi litamsonga,Lakini atawasonga wao mpaka visigino.
20 Asheri, chakula chake kitakuwa kinono,Naye atatoa tunu za kifalme.