23 Wapiga mishale walimtenda machungu,Wakamtupia, wakamwudhi,
24 Lakini upinde wake ukakaa imara,Mikono yake ikapata nguvu,Kwa mikono ya Mwenye Enzi wa Yakobo;Kwa jina la mchungaji, yeye jiwe la Israeli,
25 Naam, kwa Mungu wa baba yako atakaye kusaidia;Kwa mibaraka ya mbinguni juu.Mibaraka ya vilindi vilivyo chini,Mibaraka ya maziwa, na ya mimba.
26 Mibaraka ya baba yakoImepita mibaraka ya milima ya kale,Vitu vinavyotamanika vya vilima vya milele;Na vikae juu ya kichwa cha Yusufu,Juu ya utosi wa kichwa chake aliye mkuu kati ya ndugu zake.
27 Benyamini ni mbwa-mwitu mwenye kurarua-raruaAsubuhi atakula mawindo,Na jioni atagawanya mateka.
28 Hizo zote ndizo kabila za Israeli kumi na mbili. Na hayo ndiyo aliyowaambia baba yao, na kuwabariki; mmoja mmoja kwa mbaraka wake aliwabariki.
29 Akawaamuru, akasema, Mimi ninakwenda kukusanywa pamoja na watu wangu; mnizike pamoja na baba zangu, katika pango iliyomo shambani mwa Efroni, Mhiti;