25 Methusela akaishi miaka mia na themanini na saba, akamzaa Lameki.
26 Methusela akaishi baada ya kumzaa Lameki miaka mia saba na themanini na miwili, akazaa wana, waume na wake.
27 Siku zote za Methusela ni miaka mia kenda na sitini na kenda, akafa.
28 Lameki akaishi miaka mia na themanini na miwili, akazaa mwana.
29 Akamwita jina lake Nuhu, akinena, Huyu ndiye atakayetufariji kwa kazi yetu na kwa taabu ya mikono yetu katika nchi aliyoilaani BWANA.
30 Lameki akaishi baada ya kumzaa Nuhu miaka mia na tisini na mitano, akazaa wana, waume na wake.
31 Siku zote za Lameki ni miaka mia saba na sabini na saba, akafa.