7 BWANA ni mwema, ni ngome siku ya taabu; naye huwajua hao wamkimbiliao.
8 Lakini kwa gharika ifurikayo atapakomesha kabisa mahali pake, na kuwafuatia adui zake hata gizani.
9 Mnawaza nini juu ya BWANA? Yeye atakomesha kabisa; mateso hayatainuka mara ya pili.
10 Kwa maana wangawa kama miiba iliyotatana, na kunyweshwa kana kwamba ni katika kunywa kwao, wataliwa kabisa kama mabua makavu.
11 Ametoka mmoja kwako, aniaye mabaya juu ya BWANA, atoaye mashauri yasiyofaa kitu.
12 BWANA asema hivi, Ijapokuwa wana nguvu zilizo timilifu, ijapokuwa ni wengi, hata hivyo watakatwa, naye atapita na kwenda zake. Ingawa nimekutesa, sitakutesa tena.
13 Na sasa nitakuvunjia nira yake, nami nitakupasulia mafungo yako.