11 Tena utalewa, utafichwa; tena utatafuta ngome kwa sababu ya adui.
12 Ngome zako zote zitakuwa kama mitini yenye tini zilizoiva kwanza; ikitikisika zaanguka katika kinywa chake alaye.
13 Tazama, watu wako walio ndani yako ni wanawake; malango ya nchi yako yamekuwa wazi kabisa mbele ya adui zako; moto umeteketeza mapingo yako.
14 Teka maji yawe tayari kwa kuzingirwa kwako;Zitie nguvu ngome zako;Ingia katika udongo, yakanyage matope,Itie nguvu tanuru ya kuokea matofali.
15 Huko moto utakuteketeza;Upanga utakukatilia mbali;Utakumeza kama tunutu alavyo;Jifanye kuwa wengi kama tunutu!Jifanye kuwa wengi kama nzige!
16 Umeongeza wafanya biashara wako kuwa wengi kuliko nyota za mbinguni; tunutu huharibu; kisha huruka juu na kwenda zake.
17 Watu wako waliotiwa taji ni kama nzige, na majemadari wako ni kama makundi ya mapanzi, watuao katika vitalu siku ya baridi, lakini jua lipandapo huruka juu na kwenda zao, na mahali pao walipo hapajulikani.