3 Nikawaambia, Yasifunguliwe malango ya Yerusalemu kabla halijachomoza jua; nao walinzi wangali wakisimama bado, waifunge milango, mkaikaze; kisha wekeni walinzi wa zamu wa hao wakaao Yerusalemu, kila mtu na zamu yake, na kila mtu kuielekea nyumba yake.
4 Basi mji ulikuwa wa nafasi nyingi, tena mkubwa; lakini watu waliomo walikuwa haba, wala nyumba hazijajengwa.
5 Mungu wangu akanitia moyoni mwangu, kwamba niwakusanye wakuu na mashehe, na watu, ili wahesabiwe kwa nasaba.Nikakiona kitabu cha vizazi vya hao waliokwea hapo kwanza, nikaona ya kwamba imeandikwa humo;
6 Hawa ndio wana wa wilaya, waliokwea kutoka katika ule uhamisho wa hao waliokuwa wamechukuliwa, ambao Nebukadreza, mfalme wa Babeli, aliwachukua mateka, nao wakarudi Yerusalemu na Yuda, kila mtu mjini kwake;
7 ndio hawa waliokuja pamoja na Zerubabeli, Yoshua, Nehemia, Seraya, Reelaya, Nahamani, Mordekai, Bilshani, Mispari, Bigwai, Rehumu, na Baana. Hii ndiyo hesabu ya wanaume wa watu wa Israeli;
8 Wana wa Paroshi, elfu mbili mia moja sabini na wawili.
9 Wana wa Shefatia, mia tatu sabini na wawili.