69 ngamia zao, mia nne thelathini na watano; punda zao, elfu sita na mia saba na ishirini.
70 Na baadhi ya wakuu wa mbari za mababa walitoa mali kwa ajili ya kazi hii. Yule Tirshatha akatoa kwa ajili ya hazina darkoni za dhahabu elfu moja, na mabakuli hamsini, na mavazi ya makuhani mia tano na thelathini.
71 Na baadhi ya wakuu wa mbari za mababa wakatoa, na kutia katika hazina ya kazi hiyo, darkoni za dhahabu ishirini elfu, na mane za fedha elfu mbili na mia mbili.
72 Na mabaki ya watu wakatoa darkoni za dhahabu ishirini elfu, na mane za fedha elfu mbili, na mavazi ya makuhani sitini na saba.
73 Hivyo makuhani, na Walawi, na mabawabu, na waimbaji, na baadhi ya watu, na Wanethini, na Israeli wote, wakakaa mijini mwao.Hata ulipowadia mwezi wa saba, wana wa Islaeli walikuwa wakikaa katika miji yao.