19 Inuka, ulalamike usiku,Mwanzo wa makesha yake;Mimina moyo wako kama maji usoni pa Bwana;Umwinulie mikono yako;Kwa uhai wa watoto wako wachanga wazimiao kwa njaa,Mwanzo wa kila njia kuu.
20 Tazama, BWANA, uangalie,Ni nani uliyemtenda hayo!Je! Wanawake wale mazao yao,Watoto waliowabeba?Je! Kuhani na nabii wauaweKatika patakatifu pa Bwana?
21 Kijana na mzee hulala chiniKatika njia kuu;Wasichana wangu na wavulana wanguWameanguka kwa upanga;Umewaua katika siku ya hasira yako;Umeua, wala hukuona huruma.
22 Umeziita kama katika siku ya mkutano wa makini;Hofu zangu zije pande zote;Wala hapana hata mmoja aliyepona wala kusaliaKatika siku ya hasira ya BWANA;Hao niliowabeba na kuwaleaHuyo adui yangu amewakomesha.