13 Ni kwa sababu ya dhambi za manabii wakeNa maovu ya makuhani wake,Walioimwaga damu ya wenye hakiKatikati yake.
14 Hutanga-tanga njiani kama vipofu,Wametiwa unajisi kwa damu;Hata ikawa watu wasiwezeKuyagusa mavazi yao.
15 Watu waliwapigia kelele, Ondokeni, Uchafu,Ondokeni, ondokeni, msiguse;Walipokimbia na kutanga-tanga, watu walisema kati ya mataifa,Hawatakaa hapa tena.
16 Hasira ya BWANA imewatenga,Yeye hatawaangalia tena;Hawakujali nafsi za wale makuhani,Hawakuwaheshimu wazee wao.
17 Macho yetu yamechokaKwa kuutazamia bure msaada wetu;Katika kungoja kwetu tumengojea taifaLisiloweza kutuokoa.
18 Wanatuvizia hatua zetu,Hata hatuwezi kwenda katika njia zetu;Mwisho wetu umekaribia, siku zetu zimetimia;Maana mwisho wetu umefika.
19 Waliotufuatia ni wepesiKuliko tai za mbinguni;Hao walitufuatia milimani,Nao walituotea jangwani.