5 Wale waliokula vitu vya anasaWameachwa peke yao njiani;Wale waliokuzwa kuvaa nguo nyekunduWakumbatia jaa.
6 Maana uovu wa binti ya watu wangu ni mkubwaKuliko dhambi ya Sodoma,Uliopinduliwa kama katika dakika moja,Wala mikono haikuwekwa juu yake.
7 Wakuu wake walikuwa safi kuliko theluji,Walikuwa weupe kuliko maziwa;Miili yao, walikuwa wekundu kuliko marijani,Na umbo lao kama yakuti samawi.
8 Nyuso zao ni nyeusi kuliko makaa;Hawajulikani katika njia kuu;Ngozi yao yagandamana na mifupa yaoImekauka, imekuwa kama mti.
9 Heri wale waliouawa kwa upangaKuliko wao waliouawa kwa njaa;Maana hao husinyaa, wakichomwaKwa kukosa matunda ya mashamba.
10 Mikono ya wanawake wenye hurumaImewatokosa watoto wao wenyewe;Walikuwa ndio chakula chaoKatika uharibifu wa binti ya watu wangu.
11 BWANA ameitimiza kani yake,Ameimimina hasira yake kali;Naye amewasha moto katika SayuniUlioiteketeza misingi yake.