14 Nao wale wanawake wakamwambia Naomi, Na ahimidiwe BWANA, asiyekuacha leo hali huna wa jamaa aliye karibu; jina lake huyu na liwe kuu katika Israeli.
15 Naye atakurejezea uhai wako, na kukuangalia katika uzee wako; kwa maana mkweo, ambaye akupenda, naye anakufaa kuliko watoto saba, ndiye aliyemzaa.
16 Basi Naomi akamtwaa yule mtoto, akamweka kifuani pake, akawa mlezi wake.
17 Nao wale wanawake waliokuwa jirani zake wakampa jina, wakisema, Naomi amezaliwa mwana; wakamwita jina lake Obedi; yeye ndiye baba yake Yese, aliye baba yake Daudi.
18 Hivi ndivyo vizazi vya Peresi; Peresi alimzaa Hesroni;
19 na Hesroni akamzaa Ramu; na Ramu akamzaa Aminadabu;
20 na Aminadabu akamzaa Nashoni; na Nashoni akamzaa Salmoni;