11 Siku ile hutatahayarikia matendo yako yote uliyoniasi; maana hapo nitawaondoa watu wako wanaotakabari na kujivuna, wasiwe kati yako, wala hutatakabari tena katika mlima wangu mtakatifu.
12 Lakini nitasaza ndani yako watu walioonewa na maskini, nao watalitumainia jina la BWANA.
13 Mabaki ya Israeli hawatatenda uovu, wala kusema uongo; wala ulimi wa hadaa hautaonekana kinywani mwao; kwa maana watakula na kulala, wala hapana mtu atakayewaogofya.
14 Imba, Ee binti Sayuni; piga kelele, Ee Israeli;Furahi na kushangilia kwa moyo wako wote, Ee binti Yerusalemu.
15 BWANA ameziondoa hukumu zako,Amemtupa nje adui yako;Mfalme wa Israeli, naam, yeye BWANA, yu katikati yako;Hutaogopa uovu tena.
16 Katika siku ile Yerusalemu utaambiwa,Usiogope, Ee Sayuni; mikono yako isilegee.
17 BWANA, Mungu wako, yu katikati yako shujaa awezaye kuokoa;Atakushangilia kwa furaha kuu,Atakutuliza katika upendo wake,Atakufurahia kwa kuimba.