16 Katika siku ile Yerusalemu utaambiwa,Usiogope, Ee Sayuni; mikono yako isilegee.
17 BWANA, Mungu wako, yu katikati yako shujaa awezaye kuokoa;Atakushangilia kwa furaha kuu,Atakutuliza katika upendo wake,Atakufurahia kwa kuimba.
18 Nitawakusanya wanaousikitikia mkutano wa ibada, hao waliokuwa wa kwako; ambao mzigo uliokuwa juu yake ulikuwa fedheha kwao.
19 Tazama, wakati huo nitawapatiliza watu wote wanaokutesa; nami nitamponya yeye achechemeaye, nami nitamkusanya yeye aliyefukuzwa; nami nitawafanya kuwa sifa na jina, hao ambao fedheha yao ilikuwa katika dunia yote.
20 Wakati huo nitawaingizeni, na wakati huo nitawakusanya; kwa maana nitawafanya ninyi kuwa sifa na jina, miongoni mwa watu wote wa dunia, nitakapowarudisha wafungwa wenu mbele ya macho yenu, asema BWANA.