1 Tazama, u mzuri, mpenzi wangu,U mzuri, macho yako ni kama ya hua,Nyuma ya barakoa yako.Nywele zako ni kama kundi la mbuzi,Wakijilaza mbavuni pa mlima Gileadi.
2 Meno yako ni kama kundi waliokatwa manyoya,Wakipanda kutoka kuoshwa,Ambao kila mmoja amezaa mapacha,Wala hakuna aliyefiwa kati yao.
3 Midomo yako ni kama uzi mwekundu,Na kinywa chako ni kizuri;Mashavu yako ni kama kipande cha komamanga,Nyuma ya barakoa yako.
4 Shingo yako ni kama mnara wa Daudi,Uliojengwa pa kuwekea silaha;Ngao elfu zimetungikwa juu yake,Zote ni ngao za mashujaa.
5 Maziwa yako mawili ni kama wana-paa wawili,Nyuma ya barakoa yako.Ambao ni mapacha ya paa;Wakilisha penye nyinyoro.