11 Bibi arusi, midomo yako yadondoza asali,Asali na maziwa vi chini ya ulimi wako;Na harufu ya mavazi yakoNi kama harufu ya Lebanoni.
12 Bustani iliyofungwa ni umbu langu, bibi arusi,Kijito kilichofungwa, chemchemi iliyotiwa muhuri.
13 Machipuko yako ni bustani ya komamanga,Yenye matunda mazuri, hina na nardo,
14 Nardo na zafarani, mchai na mdalasini,Na miti yote iletayo ubani,Manemane na udi, na kolezi kuu zote.
15 Wewe ndiwe chemchemi ya bustani yangu,Kisima cha maji yaliyo hai,Vijito vya Lebanoni viendavyo kasi.