1 Naingia bustanini mwangu, umbu langu, bibi arusi,Nachuma manemane yangu na rihani,Nala sega la asali na asali yangu,Nanywa divai yangu na maziwa.Kaleni, rafiki zangu, kanyweni,Naam, nyweni sana, wapendwa wangu.
2 Nalikuwa nimelala, lakini moyo wangu u macho,Sikiliza! Mpendwa wangu anabisha!Nifungulie, umbu langu, mpenzi wangu,Hua wangu, mkamilifu wangu,Kwa maana kichwa changu kimelowa umande,Nywele zangu zina manyunyu ya usiku.
3 Nimeivua kanzu yangu; niivaeje?Nimeitawadha miguu; niichafueje?
4 Mpendwa wangu aliutia mkono wake tunduni,Na moyo wangu ukachomeka kwa ajili yake.
5 Nikaondoka nimfungulie mpendwa wangu;Mikono yangu ilidondoza manemane,Na vidole vyangu matone ya manemane,Penye vipini vya komeo.