12 Macho yake ni kama hua penye vijito,Wakioga kwa maziwa, wakiikalia mito iliyojaa;
13 Mashavu yake ni kama matuta ya rihani,Ambayo hufanyizwa manukato;Midomo yake ni kama nyinyoro,Inadondoza matone ya manemane;
14 Mikono yake ni kama mianzi ya dhahabu,lliyopambwa kwa zabarajadi;Kiwiliwili chake kama kazi ya pembe,Iliyonakishiwa kwa yakuti samawi;
15 Miguu yake ni kama nguzo za marimari,Zilizowekwa juu ya misingi ya dhahabu;Sura yake ni kama Lebanoni,Ni bora mfano wa mierezi;