3 Maana ulinitupa vilindini,Ndani ya moyo wa bahari;Gharika ya maji ikanizunguka pande zote;Mawimbi yako yote na gharika zako zote zimepita juu yangu.
4 Nami nikasema, Nimetupwa mbali na macho yako;Lakini nitatazama tena kukabili hekalu lako takatifu.
5 Maji yalinizunguka, hata nafsini mwangu;Vilindi vilinizunguka;Mwani ulikizinga kichwa changu;
6 Nalishuka hata pande za chini za milima;Hiyo nchi na mapingo yake yalinifunga hata milele;Lakini umeipandisha nafsi yangu kutoka shimoni,Ee BWANA, Mungu wangu,
7 Roho yangu ilipozimia ndani yangu,Nalimkumbuka BWANA;Maombi yangu yakakuwasilia,Katika hekalu lako takatifu.
8 Watu waangaliao mambo ya ubatili na uongoHujitenga na rehema zao wenyewe;
9 Lakini mimi nitakutolea sadaka kwa sauti ya shukrani;Nitaziondoa nadhiri zangu.Wokovu hutoka kwa BWANA.