11 Ikawa watu wote walipokuwa wamekwisha vuka kabisa, hilo sanduku la BWANA likavuka, na hao makuhani, mbele ya macho ya hao watu.
12 Na wana wa Reubeni, na wana wa Gadi na hiyo nusu ya kabila ya Manase, wakavuka, hali ya kuvaa silaha mbele ya wana wa Israeli, kama Musa alivyowaambia;
13 walipata kama watu arobaini elfu hesabu yao, wenye kuvaa silaha tayari kwa vita, waliovuka mbele ya BWANA, waende vitani, hata nchi tambarare za Yeriko.
14 Siku ile BWANA alimtukuza Yoshua mbele ya macho ya Israeli wote; nao wakamcha, kama walivyokuwa wakimcha Musa, siku zote za maisha yake.
15 Kisha BWANA akanena na Yoshua, akamwambia,
16 Haya, uwaamuru makuhani, hao waliolichukua sanduku la ushuhuda, kwamba wakwee juu kutoka mle katika Yordani.
17 Basi Yoshua akawaamuru hao makuhani, akawaambia, Haya, kweeni mtoke Yordani.