22 Maadamu sasa, kwa kuutii ukweli, nyinyi mmezitakasa roho zenu na kuwapenda wenzenu bila unafiki, basi, pendaneni kwa moyo wote.
23 Maana kwa njia ya neno hai la Mungu, nyinyi mmezaliwa upya, si kama watoto wa baba awezaye kufa, bali baba asiyekufa milele.
24 Kama Maandiko yasemavyo:“Kila binadamu ni kama majani,na utukufu wake wote ni kama ua la majani.Majani hunyauka na maua huanguka.
25 Lakini neno la Bwana hudumu milele.”Neno hilo ni hiyo Habari Njema mliyohubiriwa.