62 Hapo akatoka nje, akalia sana.
63 Wale watu waliokuwa wanamchunga Yesu, walimpiga na kumdhihaki.
64 Walimfunga kitambaa usoni, wakawa wanamwuliza, “Ni nani aliyekupiga? Hebu bashiri, tuone!”
65 Wakamtolea maneno mengi ya matusi.
66 Kulipokucha, kikao cha wazee wa watu kilifanyika, ambacho kilihudhuriwa na makuhani wakuu na waalimu wa sheria. Yesu akaletwa mbele ya Baraza hilo.
67 Nao wakamwambia, “Tuambie! Je, wewe ndiwe Kristo?” Lakini Yesu akawaambia, “Hata kama nikiwaambieni, hamtasadiki;
68 na hata kama nikiwaulizeni swali, hamtanijibu.