2 Huko alijaribiwa na Ibilisi kwa muda wa siku arubaini. Wakati huo wote hakula chochote, na baada ya siku hizo akasikia njaa.
3 Ndipo Ibilisi akamwambia, “Kama wewe ni Mwana wa Mungu, amuru jiwe hili liwe mkate.”
4 Yesu akamjibu, “Imeandikwa: ‘Mtu haishi kwa mkate tu.’”
5 Kisha Ibilisi akamchukua hadi mahali pa juu, akamwonesha kwa mara moja falme zote za ulimwengu. Huyo Shetani akamwambia,
6 “Nitakupa uwezo juu ya falme zote hizi na fahari zake, kwa maana nimepewa hivi vyote; nikitaka kumpa mtu ninaweza.
7 Hivi vyote vitakuwa mali yako wewe, kama ukiniabudu.”
8 Yesu akamjibu, “Imeandikwa:‘Utamwabudu Bwana Mungu wako,na kumtumikia yeye peke yake.’”