10 Umewafanya ufalme wa makuhani wamtumikie Mungu wetu,nao watatawala duniani.”
11 Kisha nikatazama, nikasikia sauti ya malaika wengi sana, idadi isiyohesabika, maelfu na maelfu. Walikuwa wamekaa kuzunguka kiti cha enzi, wale viumbe hai wanne na wale wazee;
12 wakasema kwa sauti kuu:“Mwanakondoo aliyechinjwa anastahili kupokeauwezo, utajiri, hekima, nguvu, utukufu na sifa.”
13 Nikasikia viumbe vyote mbinguni, duniani, chini ya dunia na baharini – viumbe vyote ulimwenguni – vikisema:“Kwake yeye aketiye katika kiti cha enzi,na kwa Mwanakondoo,iwe sifa na heshima na utukufu na enzi,milele na milele.”
14 Na wale viumbe hai wanne wakasema, “Amina!” Na wale wazee wakaanguka kifudifudi, wakaabudu.