2 Kama hao watu wanaomwabudu Mungu wangekuwa wametakaswa dhambi zao kweli, hawangejisikia tena kuwa na dhambi, na tambiko hizo zote zingekoma.
3 Lakini tambiko hizo hufanyika kila mwaka kuwakumbusha watu dhambi zao.
4 Maana damu ya fahali na mbuzi haiwezi kamwe kuondoa dhambi.
5 Ndiyo maana Kristo alipokuwa anakuja ulimwenguni, alimwambia Mungu:“Hukutaka tambiko wala sadaka,lakini umenitayarishia mwili.
6 Sadaka za kuteketezwa au za kuondoa dhambi hazikupendezi.
7 Hapo nikasema:‘Niko hapa, ee Mungu, kutimiza matakwa yakokama ilivyoandikwa juu yangu katika kitabu cha sheria.’”
8 Kwanza alisema: “Hutaki wala hupendezwi na tambiko, sadaka za kuteketezwa na za kuondoa dhambi.” Alisema hivyo ingawa sadaka hizi zote hutolewa kufuatana na sheria.