13 Na chochote mtakachoomba kwa jina langu nitafanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana.
14 Mkiniomba chochote kwa jina langu, nitawafanyieni.
15 “Mkinipenda mtazishika amri zangu.
16 Nami nitamwomba Baba naye atawapeni Msaidizi mwingine, atakayekaa nanyi milele.
17 Yeye ni Roho wa ukweli. Ulimwengu hauwezi kumpokea kwa sababu hauwezi kumwona wala kumjua. Lakini nyinyi mnamjua kwa sababu anabaki nanyi na yu ndani yenu.
18 “Sitawaacha nyinyi yatima; nitakuja tena kwenu.
19 Bado kidogo nao ulimwengu hautaniona tena, lakini nyinyi mtaniona; na kwa kuwa mimi ni hai, nanyi pia mtakuwa hai.