12 Kadhalika bawa moja la kiumbe wa pili liligusa ukuta upande mwingine wa chumba na la pili likagusana na la kiumbe wa kwanza katikati ya chumba.
13 Urefu wa mabawa mawili ya viumbe hawa ni mita 4.5. Yalisimama sambamba, nyuso za viumbe wenye mabawa zikielekea ukumbini.
14 Alitengeneza pazia kwa kitambaa cha kitani safi, cha rangi ya samawati, ya zambarau na nyekundu. Alilinakshi kwa michoro ya viumbe wenye mabawa.
15 Mfalme Solomoni alitengeneza nguzo mbili za shaba, kila moja yenye urefu wa mita 15.5, akaziweka mbele ya nyumba. Kila nguzo ilikuwa na taji juu yake yenye urefu wa mita 2.2.
16 Alitengeneza namna ya mapambo ya mikufu juu ya vichwa vya nguzo hizo, akachonga pia michoro ya makomamaga 100 juu yake.
17 Alizisimamisha nguzo hizo kwenye sebule ya hekalu, moja upande wa kusini, na nyingine upande wa kaskazini; ile ya upande wa kusini aliita Yakini, na ya upande wa kaskazini akaiita Boazi.