1 Yafuatayo ni maneno ya mwisho ya Daudi. Ni ujumbe wa Daudi mwana wa Yese; ujumbe wa mtu ambaye Mungu alimfanya awe mkuu. Mungu wa Yakobo alimteua Daudi kuwa mfalme na maneno yake Waisraeli walifurahi kuyaimba.
2 “Roho ya Mwenyezi-Mungu imesema kwa njia yangu,aliyaweka maneno yake kinywani mwangu.
3 Mungu wa Israeli amesema,Mwamba wa Israeli ameniambia,‘Mtu anapowatawala watu kwa haki,atawalaye kwa kumcha Mungu,
4 yeye ni kama mwanga wa asubuhi,jua linapochomoza asubuhi isiyo na mawingu;naam, kama mvua inayootesha majani ardhini’.
5 Hivyo ndivyo Mungu alivyoujalia ukoo wangu.Maana amefanya nami agano la kudumu milele;agano kamili na thabiti.Naye atanifanikisha katika matakwa yangu yote.
6 Lakini wasiomcha Munguwote ni kama miiba inayotupwa tu,maana haiwezi kuchukuliwa kwa mkono;