62 Hao walitafuta orodha yao katika kumbukumbu za koo, lakini hawakuonekana humo. Kwa hiyo hawakuruhusiwa kushika ukuhani kwani walihesabiwa kuwa najisi.
63 Mtawala akawaambia kuwa hawaruhusiwi kushiriki chakula kitakatifu sana, mpaka awepo kuhani atakayeweza kutoa kauli ya Urimu na Thumimu.
64 Watu wote waliorudi kutoka uhamishoni jumla yao ilikuwa 42,360;
65 mbali na hao, kulikuwa na watumishi wanaume na wanawake 7337; na walikuwa na waimbaji wanaume na wanawake, wote 200.
66 Walikuwa na farasi 736, nyumbu 245,
67 ngamia 435, na punda 6,720.
68 Watu hao waliotoka uhamishoni, walipofika kwenye nyumba ya Mwenyezi-Mungu mjini Yerusalemu, baadhi ya viongozi wa koo hizo walitoa matoleo ya hiari ili kusaidia ujenzi wa nyumba ya Mungu katika Yerusalemu.