10 Milima ilikuona, ikanyauka;mafuriko ya maji yakapita humo.Vilindi vya bahari vilinguruma,na kurusha juu mawimbi yake.
11 Jua na mwezi vilikaa kimya katika makazi yao,vilipoona miali ya mishale yako ikienda kasi,naam, vilipouona mkuki wako ukimetameta.
12 Kwa ghadhabu ulipita juu ya nchi,uliyakanyaga mataifa kwa hasira yako.
13 Ulitoka kwenda kuwaokoa watu wako,kumwokoa yule uliyemweka wakfu kwa mafuta.Ulimponda kiongozi wa jamii ya waovu,ukawaangamiza kabisa wafuasi wake.
14 Amiri jeshi ulimchoma mishale yako,jeshi lilipokuja kama kimbunga kututawanya,wakijigamba kuwaangamiza maskini mafichoni mwao.
15 Kwa farasi wako ulitembea juu ya bahari,bahari inayosukwasukwa na mawimbi.
16 Nasikia hayo nami ninashtuka mwilini,midomo yangu inatetemeka kwa hofu;mifupa yangu inateguka,miguu yangu inatetemeka.Ninangojea kwa utulivu siku ile ya maafa,ambayo inawajia wale wanaotushambulia.