1 “Tegeni masikio enyi mbingu:Sikiliza, ee dunia, maneno ninayosema.
2 Mafundisho yangu na yatone kama mvua,maneno yangu yadondoke kama umande,kama manyunyu kwenye mimea michanga,kama mvua nyepesi katika majani mabichi.
3 Maana nitalitangaza jina la Mwenyezi-Mungu,nanyi mseme, ‘Mungu wetu ni Mkuu’.
4 “Mwenyezi-Mungu ni Mwamba wa usalama;kazi zake ni kamilifu,njia zake zote ni za haki.Yeye ni Mungu mwaminifu asiye na kosa,yeye hufanya mambo ya uadilifu na ya haki.
5 Lakini nyinyi mmekosa uaminifu kwake,nyinyi sio watoto wake tena kwa sababu ya uovu,nyinyi ni kizazi kiovu na kipotovu.
6 Mnawezaje kumlipa hivyo Mwenyezi-Mungu,enyi watu wapumbavu na msio na akili?Je, yeye siye Baba yenu aliyewaumba,aliyewafanya na kuwaimarisha?