14 Aliwapa siagi na maziwa ya mifugo,mafuta ya wanakondoo na kondoo madume,makundi ya mifugo ya Bashani na mbuzi.Aliwapa ngano nzuri kabisa na divai mpya wakanywa.
15 Watu wa Israeli walinona na kupiga mateke;walinenepa, wakawa na kitambi na kunawiri;kisha wakamwacha Mungu aliyewaumba,wakamdharau Mwamba wa wokovu wao.
16 Walimfanya aone wivu mkali kwa miungu yao,walimchochea akasirike kwa matendo yao ya kuchukiza.
17 Walitambikia majini ambayo hayakuwa miungu,waliiendea miungu ambayo hawakuijua kamwe,miungu mipya iliyotokea siku za karibuni,ambayo wazee wao hawakuiheshimu kamwe.
18 Hamkumjali Mwamba aliyewapa uhai,mlimsahau Mungu aliyewazaa nyinyi.
19 Mwenyezi-Mungu aliona jambo hilo akawaacha;aliwakataa watoto wake, waume kwa wake.
20 Akasema, ‘Nitawaficha uso wangunione mwisho wao utakuwaje!Maana wao ni kizazi kipotovu,watoto wasio na uaminifu wowote.