17 Walitambikia majini ambayo hayakuwa miungu,waliiendea miungu ambayo hawakuijua kamwe,miungu mipya iliyotokea siku za karibuni,ambayo wazee wao hawakuiheshimu kamwe.
18 Hamkumjali Mwamba aliyewapa uhai,mlimsahau Mungu aliyewazaa nyinyi.
19 Mwenyezi-Mungu aliona jambo hilo akawaacha;aliwakataa watoto wake, waume kwa wake.
20 Akasema, ‘Nitawaficha uso wangunione mwisho wao utakuwaje!Maana wao ni kizazi kipotovu,watoto wasio na uaminifu wowote.
21 Wamenichochea kuona wivu kwa kitu kisicho mungu,wamenikasirisha kwa sanamu zao.Hivyo nitawafanya waone wivu kwa kisicho watu,nitawakasirisha kwa kutumia taifa la wapumbavu.
22 Hasira yangu imewaka moto,inachoma mpaka chini kuzimu,itateketeza dunia na vilivyomo,itaunguza misingi ya milima.
23 Nitarundika maafa chungu nzima juu yao,nitawamalizia mishale yangu.