31 Hata adui zetu wenyewe wamekiri wazi,mwamba wao hauna nguvu kama mwamba wetu.
32 Maana mizabibu yao ni miche ya Sodomazimetoka katika konde za Gomora;zabibu zake ni zabibu zenye sumu,vishada vyake ni vichungu.
33 Divai yao ni kama sumu ya nyoka,ina sumu kali ya majoka.
34 “Je sina njia ya kuwaadhibu?Silaha zangu ninazo mkononi.
35 Kisasi ni juu yangu,mimi nitalipiza,wakati miguu yao itakapoteleza;maana siku yao ya maafa imewadia,mwisho wao u karibu sana.
36 Mwenyezi-Mungu atawatetea watu wake,na kuwahurumia watumishi wake,wakati atakapoona nguvu zao zimeishia,wala hakuna aliyebaki, mfungwa au mtu huru.
37 Ndipo Mwenyezi-Mungu atakapowauliza watu wake,‘Iko wapi ile miungu yenu,mwamba mlioukimbilia usalama?’