34 “Je sina njia ya kuwaadhibu?Silaha zangu ninazo mkononi.
35 Kisasi ni juu yangu,mimi nitalipiza,wakati miguu yao itakapoteleza;maana siku yao ya maafa imewadia,mwisho wao u karibu sana.
36 Mwenyezi-Mungu atawatetea watu wake,na kuwahurumia watumishi wake,wakati atakapoona nguvu zao zimeishia,wala hakuna aliyebaki, mfungwa au mtu huru.
37 Ndipo Mwenyezi-Mungu atakapowauliza watu wake,‘Iko wapi ile miungu yenu,mwamba mlioukimbilia usalama?’
38 Iko wapi hiyo miungu iliyokula matoleo yenuna kunywa divai na tambiko zenu za kinywaji?Basi na iinuke, iwasaidieni;acheni hiyo iwe kinga yenu sasa!
39 Oneni kuwa mimi ndimi Munguna wala hakuna mwingine ila mimi.Mimi huua na kuweka hai;hujeruhi na kuponya,na hakuna awezaye kumwokoa yeyote mikononi mwangu.
40 Nanyosha mkono wangu mbinguni,na kuapa, kwa uhai wangu wa milele,