35 Kisasi ni juu yangu,mimi nitalipiza,wakati miguu yao itakapoteleza;maana siku yao ya maafa imewadia,mwisho wao u karibu sana.
36 Mwenyezi-Mungu atawatetea watu wake,na kuwahurumia watumishi wake,wakati atakapoona nguvu zao zimeishia,wala hakuna aliyebaki, mfungwa au mtu huru.
37 Ndipo Mwenyezi-Mungu atakapowauliza watu wake,‘Iko wapi ile miungu yenu,mwamba mlioukimbilia usalama?’
38 Iko wapi hiyo miungu iliyokula matoleo yenuna kunywa divai na tambiko zenu za kinywaji?Basi na iinuke, iwasaidieni;acheni hiyo iwe kinga yenu sasa!
39 Oneni kuwa mimi ndimi Munguna wala hakuna mwingine ila mimi.Mimi huua na kuweka hai;hujeruhi na kuponya,na hakuna awezaye kumwokoa yeyote mikononi mwangu.
40 Nanyosha mkono wangu mbinguni,na kuapa, kwa uhai wangu wa milele,
41 kama mkiuona upanga wangu umeremetao,na kunyosha mkono kutoa hukumu,nitawalipiza kisasi maadui zangu,nitawaadhibu wale wanaonichukia.