4 Mose alituamuru tutii sheria;kitu cha thamani kuu cha taifa letu.
5 Mwenyezi-Mungu akawa mfalme wa Israeli,wakati viongozi wao walipokutana,na makabila yote yalipokusanyika.
6 Mose alisema juu ya kabila la Reubeni:“Reubeni aishi wala asife,na watu wake wasiwe wachache.”
7 Juu ya kabila la Yuda alisema:“Ee Mwenyezi-Mungu usikilize kilio cha kabila la Yuda;umrudishe tena kwa watu wale wengine.Upigane kwa mikono yako kwa ajili yake,ulisaidie kabila la Yuda dhidi ya adui zake.”
8 Juu ya kabila la Lawi, alisema:“Ee Mwenyezi-Mungu ulipatie Lawi kauli yako ya Urimu,kauli yako ya thumimu kwa hao waaminifu wako,ambao uliwajaribu huko Masa.
9 Ulishindana nao kwenye maji ya Meriba.Walawi walioamua kuwaacha wazee wao,wakawasahau jamaa zao,wasiwatambue hata watoto waomaana walizingatia amri zako,na kushika agano lako.
10 Na wawafundishe wazawa wa Yakobo maagizo yako;wawafundishe watu wa Israeli sheria yako.Walawi na wafukize ubani mbele yako,sadaka nzima za kuteketezwa madhabahuni pako.