1 Jishughulishe na biasharahata kama kwa kubahatisha;yawezekana baadayeukapata chochote kile.
2 Wagawie watu saba hata wanane sehemu yako,maana, hujui balaa litakalofika duniani.
3 Mawingu yakijaa maji, mvua hunyesha;mti ukiangukia kusini au kaskazini,hapo uangukiapo ndipo ulalapo.
4 Anayengoja upepo hatapanda mbegu,anayesubiri mawingu yatoweke, hatavuna kitu.
5 Usivyojua jinsi uhai unavyoingia katika mifupa ya mtoto tumboni mwa mamake, kadhalika huwezi kuelewa matendo ya Mungu, ambayo hufanya kila kitu.
6 Panda mbegu asubuhi na jioni usiache kupanda, maana, hujui zipi zitaota; za asubuhi, za jioni, au zote zitakuwa nzuri.
7 Mwanga wafaa, na kuliona jua kwapendeza macho.