1 Nani aliye kama mwenye hekima?Nani ajuaye hali halisi ya vitu?Hekima humletea mtu tabasamu,huubadilisha uso wake mwenye huzuni.
2 Tii amri ya mfalme, kwa sababu ya kiapo chako kitakatifu.
3 Usifanye haraka kuondoka mbele yake; wala usiwe na kiburi juu ya jambo baya, maana mfalme hufanya apendavyo.
4 Amri ya mfalme ni kauli ya mwisho; nani athubutuye kumwuliza, “Unafanya nini?”
5 Anayetii amri hatapata madhara, na mwenye hekima atajua kuna wakati na njia.
6 Naam, kila kitu kina wakati wake na njia yake, ingawa binadamu anakabiliwa na tatizo kubwa:
7 Hajui ni nini kitakachotukia baadaye, kwani nani awezaye kumjulisha yatakayotukia baadaye?