2 Mwenyezi-Mungu anamrudishia Yakobo fahari yake,naam, anawapa tena Waisraeli fahari yao,ingawa wavamizi hawakuwaachia kitu,hata matawi yao ya mizabibu waliyakata.
3 Ngao za mashujaa wake ni nyekundu,askari wake wamevaa mavazi mekundu sana.Magari yao ya farasi yanamulika kama miali ya moto,yamepangwa tayari kushambulia;farasi hawatulii kwa uchu wa kushambulia.
4 Magari ya farasi yanatimua mbio barabarani,yanakwenda huko na huko uwanjani.Yanamulika kama miali ya moto!Yanakwenda kasi kama umeme.
5 Sasa anawaita maofisa wake,nao wanajikwaa wanapomwendea;wanakwenda ukutani himahimakutayarisha kizuizi.
6 Vizuizi vya mito vimefunguliwa,ikulu imejaa hofu.
7 Mji uko wazi kabisa,watu wamechukuliwa mateka.Wanawake wake wanaomboleza,wanalia kama njiwa,na kujipigapiga vifuani.
8 Ninewi ni kama bwawa lililobomoka,watu wake wanaukimbia ovyo.“Simameni! Simameni!” Sauti inaita,lakini hakuna anayerudi nyuma.