27 Hasar-shuali na Beer-sheba pamoja na vijiji vilivyoizunguka.
28 Wengine walikaa katika mji wa Ziklagi, Mekona na vijiji vilivyoizunguka.
29 Wengine walikaa katika miji ya Enrimoni, Sora, Yarmuthi,
30 Zanoa na Adulamu pamoja na vijiji vilivyoizunguka, Lakishi na mashamba yaliyouzunguka, na katika Azeka pamoja na vijiji vilivyouzunguka. Hii ina maana kwamba watu wa Yuda walikaa katika eneo lililoko kati ya Beer-sheba upande wa kusini na Bonde la Hinomu upande wa kaskazini.
31 Watu wa kabila la Benyamini walikaa Geba, Mikmashi, Ai, Betheli na vijiji vinavyoizunguka.
32 Wengine walikaa Anathothi, Nobu, Anania,
33 Hazori, Rama, Gitaimu,